Thursday, 12 November 2015

UNATAKA KUMILIKI BIASHARA? PITA HAPA...

Je, wewe ni mtu mwenye ndoto za kumiliki biashara yako mwenyewe? Unataka kuwa bosi wewe mwenyewe? Je, ni ngumu? Bila shaka. Changamoto je? Lazima zitakuwepo. Unahitaji utajiri, elimu na wasifu mrefu? Hapana. Sasa unafanyaje? Jipange!
Kuendesha biashara yako mwenyewe ni chaguo zuri kikazi na kimaisha. Inahitaji muda na malengo yako. Anza kwa kutambua kwamba unatakiwa kujitoa kikamilifu katika kuanzisha kazi yako mpaka itakapokuwa imesimama imara.
Kuna faida nyingi za kuendesha biashara yako mwenyewe.
✸✸ Uhuru na kubadilika: Uhuru wa kufanya kazi wakati na mahali popote unapotaka. Unaamua kile unachotaka mwenyewe.
✸✸ Fuata ndoto zako: Chagua biashara kulingana na kile unachopenda kukifanya na ambacho kinaendana na uwezo na ujuzi wako. Kila siku inakuwa na nafasi mpya ya kukuza uwezo na ujuzi na kufikia malengo yako.
✸✸ Kiwango cha kipato: Kipato unachoingiza kinategemea juhudi zako na kufanikiwa kwa biashara yako, jambo ambalo si kawaida sana unapokuwa umeajiriwa.
Si Kazi Ndogo
Yafuatayo ni mambo manne muhimuya kuzingatia ili kuanza biashara:
✸✸ Wazo zuri
✸✸ Maarifa/Uwezo 
✸✸ Hamasa na msukumo
✸✸ Rasilimali (za kifedha na zisizo za kifedha)
Wazo zuri
Wazo zuri ni kile kitu ambacho unaweza kukifanya na kupata faida na kufikia uhitaji wa wateja wako.
✸✸ Tambua mahitaji ya watu, ambayo hakuna mtu mwingine anayatoa.
✸✸ Ni bidhaa gani utauza au huduma unayoweza kuitoa vizuri zaidi ya mtu mwingine?
✸✸ Je, bidhaa yako itawashawishi watu kuja kuinunua na kukuletea faida?
✸✸ Fikiria hasara: Unafanya hiyo biashara kutegemea hali ya hewa au unategemea uwezo au maarifa ya watu wengine?
Maarifa na uwezo
Maarifa ni nguvu, hivyo kile unachojua kuhusu biashara yako kitakupa nguvu kuweza kufanikiwa. Kama mmiliki wa biashara ndogo, unatakiwa kujua biashara unayotaka kuianzisha; kwa mfano, unataka kuanzisha saluni ya kukata nywele, lazima uwe unajua jinsi nywele zinavyonyolewa, vifaa gani vinatumika na kama ikiwezekana wewe mwenyewe ujue jinsi ya kunyoa. Unaweza kujifunza maarifa haya kwa uzoefu rasmi au usio rasmi, elimu mafunzo, mazoezi au kujiendeleza kiujuzi. Kama huna maarifa na uwezo wowote, unapaswa kuhamasishwa ujifunze
Msukumo na hamasa
Una nafasi kubwa ya kufanikiwa kama unalipenda wazo lako na una nia ya kuliendeleza. Unatakiwa kupenda wazo la biashara unalolifikiria. Unahitaji nguvu na msukumo kuanzisha na kuendesha biashara. Unatakiwa uwe tayari kwa ajili ya hasara ambazo unaweza kukumbana nazo.
“Mtazamo wa kijasiriamali unahitajika.” Hii inamaanisha kwamba utakumbana na changamoto ambazo unatakiwa kuwa tayari kuzikabili, pia kuna mambo mengine yanakuja kwa kushtukiza. Unapaswa kuzichukulia changamoto zote kama nafasi ya kutafuta njia ya kutatua nyingine siku zijazo. Wapo watu wachache wenye bahati ya kufanikiwa chapchap katika biashara zao, lakini wapo wengi pia ambao huwachukua miaka kuweza kupata mafanikio kama hayo. Fanya biashara yako kwa bidii, kuwa makini, jifunze mbinu bora za kutunza fedha, omba msaada na ushauri kutoka katika vyanzo vya kuaminika.
Rasilimali
Ni muhimu kujua gharama za kuendeleza biashara yako. Unatakiwa kujua ni shilingi ngapi zinahitajika kupata bidhaa na au kutoa huduma yako. Bajeti yako lazima ijumuishe gharama za kuanzia, kama vifaa, sehemu ya kufanyia biashara, kodi na huduma, usafi rishaji wa bidhaa, mishahara ya wafanyakazi, malipo ya mkopo, ada ya benki, ushuru na kadhalika. Gharama ikiwa ndogo inakuwa rahisi kuanza.
Kujua gharama ya biashara yako ni muhimu ili kuamua kama inaweza kukupa faida. Ili biashara ikue, utahitaji kutengeza fedha nyingi zaidi ya ulizowekeza.
Mipango ya biashara yako
Baada ya kuhakikisha wazo lako, unahitaji kuandaa mpango wa biashara yako. Huu ni mwongozo unaokuelekeza jinsi ya kulifanyia kazi wazo lako kwa vitendo. Mipango inajumuisha malengo, mikakati na utendaji.
Andika bajeti
Bajeti yako iwe na makadirio ya mapato na matumizi kwa kipindi cha angalau miezi sita. Unatakiwa kuandika kiwango cha fedha unachohitaji kila siku, kila wiki, kila mwezi kuendesha biashara yako. Andika ni kiasi gani cha fedha kinahitajika kwa gharama zote. Unapoanza biashara kuwa mkweli. Unaweza usifi kie matarajio yako yote kwa wiki au mwezi wa kwanza, hivyo unatakiwa kuweka bajeti ya gharama zako hadi uinuke na kuweza kuiendesha.
Yaliyomo kwenye mipango
Inajumuisha mambo mengi:
Maelezo ya biashara: Nini cha kufanya, kuzalisha au kuuza?
Utafiti wa soko: Ni kina nani unakwenda kuwauzia bidhaa zako au kuwapa huduma?
Uchambuzi wa soko: Kwa nini watanunua bidhaa zako au kufuata huduma zako? Ni kwa sababu una huduma na bidhaa bora zaidi ya wengine? Ni sehemu gani nyingine wanaweza kupata huduma hiyo?
Utekelezaji: Utatoaje huduma yako? Wakati gani? Mahali gani? Utawafi kiaje wateja wako?
Changamoto: Ni vikwazo gani vinaweza kujitokeza? Utatuaje? Je, kuna watu ambao wanaweza kukusaidia?
Kutafuta njia ya kupata fedha
Unaweza kuhitaji kuwa na fedha ya kuanzia. Vifutav yo ni vyanzo vinavyoweza kukusaidia.
✸ Akiba yako
✸ Familia
✸ Vyama vya kuweka na kukopa visivyo toa riba
✸ Benki za biasharabila riba
✸ Mikopo midogo ya biashara kutoka kwa watu binafsi 
✸ Ruzuku .

SOURES FEMA HIP

KIPI NI BORA KATI YA WAZO LA BIASHARA AU MTAJI???TUNDIKIE MAONI YAKO







No comments:

Post a Comment