Saturday, 7 November 2015

IPI HISTORIA YA UJASIRIAMALI????

Historia ya Elimu ya Ujasiriamali
Asili ya elimu ya ujasiriamali katika vyuo na vyuo vikuu ilianzia Marekani ambapo kozi ya kwanza ya MBAilianzishwa mwaka1947 katika Shule Kuu ya Biashara ya Harvard chini ya kichwa cha habari “Uendeshajiwa Biashara Mpya” (Katz 2003). Kuanzia miaka ya 1980 na kuendelea, elimu ya ujasiriamali ilianza kuenea kwanza Ulaya Kaskazini, na kisha kuenea katika sehemu za Ulaya ya Kati na Ulaya ya Kusini katikamiaka ya 1990. Elimu ya ujasiriamali baadaye ilienea katika sehemu zingine za dunia. Kimataifa, Amerikaya Kaskazini ndio mfano wa kuigwa katika ustawi wa miradi na pia Amerika ya Kaskazini ni kiongozikatika elimu ya ujasiriamali. Hakuna asiyejua mchango mkubwa wa kiuchumi wa Kampuni ya Microsoft, Amazon, Intel, Cisco au Google na makampuni mengine yenye ustawi mkubwa huko Marekani.Ukilinganisha na nchi zingine, Marekani ndiyo nchi yenye historia kubwa katika elimu ya ujasiriamali, napia ndiyo nchi yenye mpangilio, utamaduni na mazingira rafiki ya ujasiriamali kuliko nchi yoyote duniani(Kourilloff, 2000).Nchini Tanzania, elimu ya ujasiriamali haikuwepo enzi za ujamaa wakati wa Azimio la Arusha.Wakati huo Watanzania walisadikishwa kuchukia kila kitu kinachohusiana na ubepari, ujasiriamali ukiwemo.Mjasiriamali alichukuliwa ni kama shetani na alilinganishwa na mnyama katili wa mwituni. Msemo“Ubepari ni Unyama” ulisikika kwenye radio kila baada ya taarifa ya habari. Ujasiriamali uliwavutia tu waleambao walichukuliwa kuwa ni watu waliopotoka kimaadili. Watumishi wa umma walizuiwa kujishughulisha na biashara (Rutihinda, 2002). Kwa kuwa karibu watumishi wote wa umma walikuwa ni Waafrika, hiiina maanisha kuwa shughuli za kibiashara zilibaki kuwa za Watanzania wenye asili ya Asia pamoja na walewazawa ambao walikuwa hawana ajira katika ofisi za umma. Watu wa aina hii walikuwa ni wale ambaohawakuwa na kiwango kikubwa cha elimu (Olomi, 2009). Hata hivyo, maendeleo ya hivi karibuni katika

No comments:

Post a Comment