Wengi wetu tunapenda kushiriki katika kufanikisha jambo fulani kubwa
na hata kujumuika na wenzetu wanaotuzunguka. Kwa jinsi tulivyojifunza
baada ya kukutana na watu wengi wanaojitolea, tunaona kwamba kujitolea
ni namna mojawapo na nzuri zaidi ya kutuwezesha kufanilisha azma hii.
Nani anajitolea?
Kuna aina nyingi tofauti za watu wanaojitolea, wenye misukumo na malengo tofauti. Mtu anayejitolea anaweza kuwa:
Nani anajitolea?
Kuna aina nyingi tofauti za watu wanaojitolea, wenye misukumo na malengo tofauti. Mtu anayejitolea anaweza kuwa:
-
Mtu aliyetambua mahitaji ya jamii yake na kuyashughulikia, anajisikia
kuwajibika kwa jamii, anakwenda hatua mbele zaidi ya majukumu yake ya
msingi.
-
Mtu ambaye anajitolea muda na utaalam wake kwa manufaa ya wengine na wakati huo huo akipiga hatua zaidi mbele.
-
Mtu ambaye halipwi mshahara na hatambuliki kama mwajiriwa
Kujenga ujuzi Kazi ya kujitolea inatoa fursa kwako kujifunza mambo mapya na kupata ujuzi wa kazi pamoja na kujenga hali ya kujiamini. Kefar Mbogela, (28) ni Mratibu Msaidizi wa Mradi, Restless Development. Kefar alianza kujitolea katika asasi hiyo mara baada ya kuhitimu Kidato cha Nne. Baada ya kujitolea kwa miaka mitatu pale Restless Development, hivi sasa ameajiriwa kuratibu mafunzo kuhusu masuala ya Katiba katika mikoa mbalimbali. “Nikiwa chuo kikuu niliwafundisha watu mambo yanayohusu ushiriki wa wananchi. Nimekuwa na ujasiri zaidi na nimepata uzoefu mkubwa katika zoezi hilo, sihitaji tena usimamizi kwa jambo lolote na naweza kushughulika na kundi kubwa tu wakati ninapotoa mafunzo juu ya mambo yanayoigusa nchi yetu.”
Faida za kujitolea
Tunapofi kiria kujitolea, wengi wetu tunafi kiria kufanya kazi bila kupata chochote, hata pesa. Lakini, tunapata mambo mengi na ukweli ni kwamba faida tunazozipata zina thamani zaidi ya fedha!
Kujenga ujuzi
Kazi ya kujitolea inatoa fursa kwako kujifunza mambo mapya na kupata ujuzi wa kazi pamoja na kujenga hali ya kujiamini.
Kefar Mbogela, (28) ni Mratibu Msaidizi wa Mradi, Restless Development. Kefar alianza kujitolea katika asasi hiyo mara baada ya kuhitimu Kidato cha Nne. Baada ya kujitolea kwa miaka mitatu pale Restless Development, hivi sasa ameajiriwa kuratibu mafunzo kuhusu masuala ya Katiba katika mikoa mbalimbali.
“Nikiwa chuo kikuu niliwafundisha watu mambo yanayohusu ushiriki wa wananchi. Nimekuwa na ujasiri zaidi na nimepata uzoefu mkubwa katika zoezi hilo, sihitaji tena usimamizi kwa jambo lolote na naweza kushughulika na kundi kubwa tu wakati ninapotoa mafunzo juu ya mambo yanayoigusa nchi yetu.”
Kujijenga kitaaluma
Kujitolea kunakusaidia katika kujiendeleza kitaaluma – ni fursa ya kunoa ujuzi katika masuala ya uongozi, kujiamini na kujitambua. Utaboresha utendaji wako na mwisho wa siku utapata uzoefu, jambo ambalo linakuongezea uwezekano wa kupata ajira.
Adeline Cosmas, (24), ni Mratibu Msaidizi wa Mradi, Mabinti Tushike Hatamu, mradi unaoishirikisha serikali na asasi za kiraia, unaowalenga wasichana kati ya miaka 10 na 19.
“Nilipokuwa chuo kikuu na mara baada ya kumaliza chuo, nilijitolea katika taasisi ya habari ambapo nilijifunza kufanya kazi na watu wa serikali ya mtaa, hii ilinisaidia nilipoomba kazi.”
Adeline anasema, anamshukuru baba yake ambaye alimfundisha utaalam wake wa kufundisha, aliwafundisha wasichana wa darasa la nne na la tano Kiingereza na Hisabati kwa miezi sita wakati huo akiwa na miaka 19, jambo ambalo lilimjengea moyo wa kuwasaidia wengine.
Kujenga mtandao
Uzoefu unaopatikana kwa kujitolea ni fursa pia ya kujenga mtandao wa marafi ki pamoja na kupata mawazo mapya na mtazamo tofauti wa mambo. Hawa pia ni watu ambao watakumbuka kazi uliyoifanya.
Ridhwan Ridhwan, (26), ni mwalimu wa Arusha School na ni balozi wa Fema ambaye amekuwa akijitolea kama mwelimishaji rika TACAIDS, msimamizi wa mazingira ya shule yake na mtu ambaye amekuwa akizisaidia shule katika mkoa wake kuanzisha klab za Fema. Uzoefu wake umemwezesha kukutana na watu wa kila namna.
“Kwa mitandao niliyoijenga katika shughuli zangu za kujitolea hapa Arusha na wakati nikiwa masomoni, mashirika ya kimataifa kutoka nchi mbalimbali yamekuwa yakinialika katika matukio mbalimbali baada ya kukumbuka kazi ambazo nilizifanya na baadhi ya watu wa mashirika hayo.”
Mwisho wa siku, unapotafakari ulichokifanya – unajisikia vizuri!
KUMBUKA
Jitolee ukiwa na lengo la kusaidia wengine au jamii, badala ya kufi kiria ni namna gani utanufaika kifedha. Unapojitolea, jitume kadri ya uwezo wako kwani huwezi kujua itakusaidiaje hapo baadaye.
SOURCES:Fema 31, uk. 40, na Gaure Mdee
No comments:
Post a Comment