Saturday, 7 November 2015

MABADILIKO ENDELEVU

                      GO WITH CHANGES,CHANGE WITH CONTENTS

Ulimwengu unabadilika kwa kasi kubwa. Kwa hakika jamii yoyote ambayo haijajiandaa kikamilifu kuendana na kasi ya mabadiliko hayo, kuna uwezekano wa kuwa jamii yenye kutegemea misaada. Jamii hiyohaitakuwa na mbadala zaidi ya kutembeza bakuli kwa ajili ya kuomba chochote. Na cha kusikitisha zaidi,hali hii haitaathiri kizazi kilichopo tu, bali hata kizazi kijacho ambacho hakitakuwa na uwezo wa kulipamadeni yaliyokopwa na baba zao. Kwa hali hiyo, laana ya utamaduni wa kuwa ombaomba itaendelea kuwepo kwa vizazi hadi vizazi kwa kuwa mtoto wa ombaomba ni ombaomba pia
 ONA MAAJABU:wanaomba hadi msaada wa kujengewa choo cha familia??
Tafiti zinaonesha nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa mfano, zimejaliwa raslimali ambazo zinaweza kubadilishwa kuwa mali. Lakini suala ni jinsi ya kuzigeuza raslimali hizo ili kuwa vitu halisi. Elimu isiyofaaimeelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa kinachokwamisha kuzibadilisha raslimali hizo kuwa vitu halisi.Elimu ya Tanzania inasemekana kuwa ni elimu inayowaandaa watu kuwa waajiriwa wa maofsini, japokuwanafasi za kazi ni chache ukilinganisha na idadi ya watu wanaotafuta kazi za kuajiriwa. Kwa ufupi, elimuyetu haijengi ubunifu na udadisi ambao ungewawezesha watu ama kujiajiri (ujasiriamali) au kuzipanuafursa za ajira ambazo zingewawezesha watu wengi kupata ajira. Fursa za ajira hazijatumiwa kwa kiwangokikubwa kiasi cha kuweza kuwachukua watu wote wenye sifa za kuajiriwa. 
Dhana ya ujasiriamali imeelezwa kwa namna tofautitofauti. Baadhi ya watu hufikiri kuwa ujasiriamalini kufanya biashara tu. Baadhi wanauangalia ujasiriamali katika muktadha mpana unaohusisha ujuzi namaarifa ya mtu katika kutumia fursa zilizopo. Tranchet na Rienstra, (2009), kwa mfano, wanaelezea dhanaya ujasiriamali kama uwezo binafsi wa mtu wa kubadilisha mawazo na kuwa vitendo. Ujasiriamali unajumuisha ubunifu, kutengeneza kitu kipya na kuwa tayari kukabiliana na ugumu; vilevile kuwa na uwezo wakupanga na kuendeleza miradi ili kufikia malengo. Dhana hii humsaidia mtu katika maisha yake ya kilasiku akiwa nyumbani na katika jamii. Huwafanya waajiriwa kuwa na uelewa kuhusu muktadha wa kazi zaona kuwa katika nafasi nzuri katika kutumia fursa. Pia ujasiriamali hutoa msingi kwa wajasiriamali kujengashughuli za kijamii au kibiashara. Olomi, (2009) anakubalina na dhana kuwa ujasiriamali kwa ujumla unaweza kuelezewa kama namna ya kufikiri, kutafakari na kutenda inayosababisha utengenezaji, uimarishaji,utambuzi na ufanyaji mpya wa vitu kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu na jamii.
Baadhi huelezea ujasiriamali kwa kutumia sifa za mjasiriamali. Sifa kubwa za mjasiriamali ni pamoja na :
•Kuwa tayari kupambana na hatari yoyote
•Huchukua uamuzi mapema na hasubiri tatizo likue
•Mvumbuzi
•Mbunifu
•Mwenye kuleta tija
•Mwenye kujitegemea
•Mwenye kutumia fursa zilizopo
•Mwenye kufikia malengo yako

GO OUT AND DO SOMETHING BEST YOU WILL  FILL HOPES YOURSELF AND YOU WILL  HOPES THE WORLD by barakamussa170

No comments:

Post a Comment