Tuesday, 10 November 2015

MSONGO MAWAZO(STRESS)



Msongo wa mawazo unaweza kukupelekea ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi zaidi,kukufanya kupoteza hamu ya kula. Jambo la kufurahisha ni kuwa msongo wa mawazo unaepukika, leo nimejaribu kueleza  baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kuepukana  kupata msongo wa mawazo.

                                 jizoeze kukabiliana na changamoto za maisha

Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi

Usiwaze zaidi au usikae na jambo linalo kusumbua moyoni 
Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni vyema ukamshirikisha mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu, mume au hata mshauri. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako

 Jali afya yako kiujumla
mara nyingi tunakuwa na shughuli nyingi kiasi cha kuusahau mwili na kuuchukulia tu kwa juu juu. Ni muhimu sana mwili wako uwe katika hali nzuri na afya bora ili uweze kufanya kazi zako vizuri na kwa wepesi. Hakikisha unakula chakula chenye virutubisho bora na pia unakunywa maji ya kutosha. Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na pata muda wa kutosha wa kupumzika kila siku.

Pangilia mambo yako vizuri
 hakikisha unapangilia mambo yako na shughuli zako za kila siku,hii itakusaidia sana kuepukana na msongo mawazo  ,ni muhimu kuishi kwa mpangilio ,panga maisha yako vizuri usiishi au usiongozwi na matukio

jaribu kufanya mazoezi kula matunda

hii itauweka mwili wako vizuri na kukuepusha na msongo mawazo ,faida za matoezi tembelea link hii hapahizi ni faida za kufanya mazoezi uboreshe afya na maisha yako

mungu awabariki wote!!!!!!




No comments:

Post a Comment