Soma njia 8 za kuwa huru na maisha yako.
1. Usijisikie vibaya unaposhindwa kufanya vizuri katika jambo lolote.
Unaweza kuwa umefanya vibaya sana katika kazi au mitihani uwapo shuleni, usife moyo na kukata tamaa. Ni kawaida mtu kushindwa kufanya vizuri, kila mtu ana udhaifu wake mahali fulani hivyo ukijipanga upya na kuongeza bidii katika kujifunza wapi umekosea na wapi unahitaji kutilia mkazo zaidi hapo baadae utaweza kuwa hodari na mahiri kwa kile ulichokifanyia kazi. Chukulia mapungufu yako kama ni mwalimu wa kukuonyesha makosa na udhaifu ulionao ili ujirekebishe na kuwa mtu bora.
Soma pia: Sababu 5 za wewe usikate tamaa
2. Usijutie sana kukosa nafasi au fursa ya kupata kitu ulichotegemea kupata.
Inatokea hukubahatika kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wako kuwa unaweza kufanya kitu fulani au kuonekana unastahili. Penye watu wengi wenye nia moja kila mtu anategemea kushinda kama wewe.
Mfano: Kazini wakati wa kupewa "promotion" au "bonas" kila mfanyakazi anapenda kutunukiwa zawadi hivyo haiwezekani wote mpate japokuwa unastahili. Hivyo katika hali ya watu wengi kutegemea kupata kitu kimoja jifunze kuelewa kuna kukosa au kupata.
Kujua zaidi: Soma Jinsi ya kutumia fursa zilizopo katika ajira ukiacha mshahara
3. Usikose kuwa na imani na watu.
Kuna hali ambayo ni ya kawaida kuwa na mashaka na mtu juu ya utendaji wake wa kazi au namna alivyo. Hofu yako inapozidi ni vigumu kuridhika na kazi au jambo lolote atakalofanya mtu mwingine. Kama una mashaka na mtu ni bora ukamweleza jinsi unavyotaka mambo yawe au mtafute mtu mwingine unayefikiri anawezafanya utakavyo. Hakuna mtu awezaye kufanya mambo yote mwenyewe, kugawana majukumu na kushirikiana kwa pamoja ndio mafanikio ya kuwa na mahusiano bora na utendaji mzuri wa kazi.
4. Usifikirie sana kuhusu maisha yako ya baadae kuwa mabaya.
Hakuna sababu ya kuwa na mawazo hasi (negative thoughts) kwani maisha ni safari ndefu na hubadilika kila siku kwa kadri utakavyojitahidi kupambana na maisha yako.
Ikiwa una matumaini kuwa mambo yatakwenda vizuri na kujitahidi kutafuta maisha yaliyobora kwako ni wazi kuwa utashinda. Katika maisha hakuna hali ya kudumu hivyo mambo hubadilika. Muhimu ni kujituma kwa bidii bila kuchoka au kukata tamaa.
Don't be afraid of going slow. Be afraid of standing still."
5. Usiwaze sana kwanini watu hutenda mabaya.
Duniani kuna watu wa kila aina, kwa maana ya kila mtu ana tabia au hulka yake. Kuna watu wabaya na wazuri. Kwa kulijua hilo tegemea kukutana na watu tofauti tofauti katika maisha yako. Amini kuwa kuna watu wengi wazuri lakini sio wote, hivyo uasi au ubaya wa mtu usikufanye uhuzunike au kubadilisha mtazamo wa maisha yako kwasababu unastahili kuishi kwa amani, upendo na furaha.
Makala nyingine ya kupitia: 32 Tips for living a happy and rewarding life
6. Usitamani kupita kiasi mafanikio ya mtu mwingine au kujilinganisha sana na watu wengine waliokuzidi uwezo katika nyanja fulani.
Kutamani ni chachu ya maendeleo lakini tamaa inapozidi hukufanya ukose msimamo wa namna maisha yako unavyotaka yawe. Kama mwenzako ana mafanikio makubwa na umevutiwa na maendeleo yake ni vyema ukajifunza kutoka kwake.
Hatuwezi wote kuwa na mafaniko makubwa kama matajiri wa dunia lakini tunaweza kuwa na mafanikio makubwa yaliyo bora kimaisha kulingana na matakwa yetu. Ni vyema ukawa na ufafanuzi wako wa nini maana ya mafanikio kwako iwe ni kuwa na pesa nyingi au mali tele, maendeleo binafsi ya kujiimarisha kitabia, kimahusiano n.k. Unauwezo wa kufanikiwa chochote kile unachotaka lakini itategemeana na jinsi utakavyojipanga na kujibidiisha katika utafutaji.
7. Usiogope kushindwa kwasababu wengine walishindwa au walikumbwa na matatizo.
Kila mtu ana njia yake kimaisha, hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi utashindwa ikiwa unajua kitu unachofanya sio kibaya au hakitadhuru maisha yako. Kuna mambo ya kuogopa lakini sio yote, wewe ndiye mwenye maamuzi ya nini ufanye na nini usifanye. Jaribu na ushindwe, thubutu kutenda na ushindwe lakini usife moyo na kuogopa kujaribu.
8. Usifikirie watu wengine watakuonaje iwapo utaamua kubadilika au kufanya maamuzi yako.
Wewe ndiye mmiliki wa maisha yako, rubani wa maisha yako na una kila sababu ya kufanya maamuzi unayoona yanafaa kuhusu maisha yako. Huwezi kuwa mtu bora pasipo kubadilika, huwezi kufanya mambo yenye manufaa kwako ikiwa huna maamuzi na maisha yako.
Unaweza soma pia: Siri ya kuishi maisha yenye furaha
Unapodiriki kubadilika, mwenye nafasi kubwa ya kuamua nini ufanye ni wewe. Watu wengine wanaweza kukushauri , kukusihi na kukueleza watakayo lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe. Usiogope kufanya maamuzi yako binafsi ikiwa unajiona upo sahihi kwa kile unachoamini ni sawa.
Worring changes nothing, you better decide to act or keep calm.''Kumbuka wasiwasi haubadilishi chochote, ni bora uamue kuchukua hatua au uwe mtulivu.